HUZUNI::PICHA ZA KIJANA ALIYEJINYONGA KUKWEPA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE ILIYOANZA LEO,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA.

 Mwanafunzi  aliyekuwa akisubiri kufanya  mtihani  wa kidato cha nne unaotaraji  kuanza kesho Bw Khamis Mkundo mkazi  wa Mwangata C katika Manispaa  ya Iringa  akiwa amejinyonga  usiku  huu kuhofu  mtihani  wa kidato cha nne
 Mwenyekiti  wa serikali ya mtaa wa Mwangata C Bw Sarehe Mgimwa akisoma ujumbe  ulioachwa na marehemu huyu 
 Askari  kanzu  akikagua  mwili wa mwanafunzi  huyo  


 Wananchi  wa Mwangata  mjini Iringa  wakiwa nyumbani kwa marehemu  
 Mwili  wa kijana  huyo ukitolewa  tayari  kupelekwa  chumba  cha kuhifadhia maiti Hospital  ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa
Mwili  huo ukipakiwa katika gari  la  polisi
 

Mwanafunzi  wa  aliyekuwa akisoma  shule  ya  sekondari  Sabasaba  mjini  Iringa akijiandaa kurudia  kufanya  mtihani  wa  taifa  wa kidato  cha nne kupitia  kituo  cha Krelluu mjini  Iringa Khamis Mkundo  mkazi  wa Mwangata  C katika manispaa ya  Iringa amejiua kwa kujinyonga  kwa kamba kwa kile  alichodai  kuchoshwa na kufeli  mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.

Katika  barua  yake  ndefu aliyoiandika  kijana  huyo amesema  kuwa amefanya  hivyo si kwa kujipendea  ila amechukizwa na hatua yake ya  kufeli mara kwa mara  hiyo  kuamua  kujiua ili  kuepuka na aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.

Shemeji  wa  kijana  huyo Aden Tagalile ameueleza mtandao  huu   kuwa  tukio  hilo limetokea mida ya  kati ya saa 12 na saa 1  usiku wa  leo baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda  mrefu  kwa kijana  huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea kurisiti  mtihani  wa kidato cha nne  bila mafanikio.

Kwani  alisema hajapenda  kuona anaendelea  kufeli na kuwa  yupo tayari kwa lolote  kukwepa aibu ambayo ipo mbele  yake.

Hata  hivyo kufuatia mazungumzo hayo kijana huyo aliangana na ndugu zake akiwemo kaka  yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani  hapo kabla  ya kijana  huyo kukutwa amejinyonga.

Mwenyekiti  wa serikali  ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha  kutokea kwa kifo  hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana  huyo ameuacha
 .CHANZO MATUKIO DAIMA
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment