"NAJUA WANACHOKIPENDA MASHABIKI KUTOKA KWA DIAMOND NDO MAANA NAONEKANA NOMA ZAIDI YAKE"...RICHIE MAVOKO

Hitmaker wa Roho Yangu, Richie Mavoko amesema anajua kile ambacho Diamond Platnumz anawashikia watu, na yeye anajua kipi cha kufanya, ndio maana anaonekana kuwa tishio kwake.
page
Richie Mavoko amesema alianza kumsikia Diamond tangu akiwa shule na kwamba hakatai kuwa kuna vitu alijifunza kutoka kwake.
Mimi Diamond anatoka, mimi nipo shule, kwahiyo kuna vitu vingi nimeviona, labda yeye amepitaje, amekosea nini na mimi nifanyeje ndio maana mara nyingi mimi naonekana noma kwasababu mimi nishajua wao wanataka nini. Yaani mimi nishajua anapowashkia watu halafu mimi nshajua natakiwa nifanye nini,”alisema.
Mavoko aliendelea kudai kuwa muziki wake na wa Diamond haufanani hata kidogo. “Mimi na huyo jamaa hatufanani kabisa yaani, sisi ni watu wawili tofauti. Wote tunaimba Bongo Flava, Wote tunafanya kitu kimoja lakini makoo tofauti sababu koo la Diamond sio koo langu mimi tuko tofauti kabisa.
Muimbaji huyo aliongeza kuwa hana urafiki wowote na Diamond licha ya kwamba wakikutana husalimiana.
Mimi nachoamini sina ushkaji naye, sio lazima kuwa na ushkaji naye lakini ni mtu ambaye ananijua, namjua ‘hi mambo, vipi poa, salama’ hatuna matatizo yaani.
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE