Screen Shot 2015-10-06 at 1.23.45 PM
-Wasanii wa Tanzania Ali Kiba,Fid Q na Vanessa kuwasha moto
 Wasanii nguli kutoka Tanzania wataungana na wasanii wengine 27 barani Afrika katika msimu wa tatu wa maonyesho ya  burudani ya muziki maarufu kwa jina la  Coke Studio Afrika ambalo litaanza Jumamosi wiki hii .Onyesho la mwaka huu ni tofauti na yaliyopita kwa kuwa litaendana na mabadiliko yaliyopo katika muziki duniani “Kolabo”na litarushwa na kituo cha televisheni cha Clouds kuanzia saa 12  jioni.
Meneja wa Biashara za Coca-Cola nchini Maurice Njowoka amesema kolabo ya wasanii 55 itashirikisha wasanii wawili kutoka nchi mbili tofauti kuimba nyimbo mbili za mitindo tofauti. “Mtindo wa Kolabo uliwahi kutumika hapo awali katika maonyesho ya televisheni,sinema na wakati wa kupiga muziki mchanganyiko lakini safari hii utatumika katika onyesho la Coke Studio na utawawezesha wasanii watakaoshiriki kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika kuwa wabunifu na kuboresha viwango vyao vya sauti za uimbaji”.Alisema
Screen Shot 2015-10-06 at 1.25.20 PM
Wasanii wanne kutoka Tanzania watakaokuwa kwenye Kolabo la Coke Studio mwaka ambalo onyesho lake litaanza kuonekana kwenye luninga Jumamosi ya Oktoba 10 ni Ben Pol ambaye atakuwa pamoja na mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi,Fid Q atakuwa pamoja na Maurice Kirya kutokana Uganda,Gwiji wa Bongo fleva nchini Ali Kiba atashirikiana  na Victoria Kimani kutoka nchini Kenya na Vanessa Mdee atakuwa pamoja na mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face.
Maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa Coke Studio Afrika yamekamilika na wapenzi wa muziki nchini wanasubiri kwa hamu kuwaona wanamuziki  wanaowashabikia wakiwasha moto kwa kushirikiana na wanamuziki kutoka nje ya nchi na hii inadhihirisha kuwa onyesho la Coke Studio litaacha historia ya pekee katika fani ya muziki nchini.
Screen Shot 2015-10-06 at 1.22.19 PM
Screen Shot 2015-10-06 at 1.21.43 PM