DERULO ATAKA BIFU NA 50 CENT


2EA7384600000578-0-image-a-8_1448071470868 (1)Staa wa Kibao cha Wiggle, Jason Derulo akipozi kimahaba na Daphne Joy.
NEW YORK, Marekani
HATARI! Staa wa Kibao cha Wiggle, Jason Derulo, ni kama anajitafutia matatizo baada ya kuonekana akiwa kwenye mkao wa kimahaba na Daphne Joy ambaye ni mzazi mwenzake na 50 Cent anayefahamika kwa ukorofi.

Ripoti zinasema sasa ni rasmi Jason anatoka na ex wa 50 Cent ambaye anafahamika kwa ukorofi kwenye mitandao ya kijamii, hivyo huenda akamjibu Derulo, 26, baada ya kupata taarifa za uhusiano wao.
Jason-Derulo1
Ijumaa iliyopita, Jason aliposti picha akiwa kwenye mkao wa kimahaba na Daphne katika Mtandao wa Instagram huku Mtandao wa TMZ ukiandika kuwa hao ni wapenzi rasmi na uhusiano wao ulianza wiki chake zilizopita baada ya kukutana huko Uingereza.

Huu ni uhusiano wa kwanza kuwa wazi kwa Jason baada ya kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu, Jordin Sparks.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment