Na Mwandishi Wetu.
MANDOJO na DOMOKAYA ni wasanii walioweza kutengeneza namna tofauti ya uwasilishwaji wa mziki wa TANZANIA (BONGO FLAVOUR) kwa matumizi ya 'Guitor'
mbali na falsafa iliyopatikana katika kazi sambamba na ustadi
ulioonekana kati yao hawa jamaa ambao walishawahi kufanya kazi
mbalimbali zilizofanya vizuri ikiwemo 'Nikupe', 'Wanoknok' na 'Dingi'.
Wakati
huu watu hawa kila mmoja anaishi nyumbani kwake kutokana na namna mfumo
wa maisha ya binadamu ulivyojengwa. Hasa ikiwa ni watu wazima na
kuhitaji kuwa na familia na mambo mengine kama hayo, DOMO aliita "KIUTU UZIMA".
Mbali na hilo, 'Mandojo' na 'Domokaya' wanamiliki duka la viatu vya wanawake linalopatikana maeneo ya 'KARIAKOO' karibu na DDC. Pia wanamiliki studio ya mziki inayofahamika kama 'VAKU RECORDS' kama ilivyoelezwa na DOMOKAYA alipokuwa akijibu swali kutoka kwa 'KAD GO' aliyekusudia kufahamu nini mwelekeo wa watu hawa wawili katika masuala ya mziki pamoja na maisha yao siku ya Jumamosi 07 NOV. ndani ya 'NEW MSASANI CLUB - KILINGE'.
Katika
kuwaridhisha mashabiki wake alijikuta akijibu swali lililoulizwa juu ya
nini mtazamo wake katika msimamo na muelekeo wa mziki wa 'BONGO HIP HOP' ikiwa imeonekana wazi wasanii wa mziki wa 'BONGO FLAVOUR' kupewa nafasi zaidi na kuibuka kidedea katika vinyang'anyilo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
"Sidhani kama mtu akifanya kitu kizuri kitapingwa, ukweli haufichiki na mtu yeyote akifanya kitu kizuri hakipingwi" Alisema.
Mbali
na imani hiyo bado aliongeza na kulalamikia mamlaka juu ya namna
anavyojishughulisha katika mziki japokuwa mpaka leo hajapata TUZO licha ya kuonekana ni msanii bora Tanzania.
0 comments:
Post a Comment