KALA JEREMIAH SASA KUWA WA KIMATAIFA

KALLAJEREMIAH1
Staa wa muziki wa hip hop nchini, Kala Jeremiah.
Sweetbert lukonge, Dar es Salaam
STAA wa muziki wa hip hop nchini, Kala Jeremiah, ameamua kupanua wigo wa muziki wake baada ya kuanza harakati za kuhakikisha anatusua kimataifa.
Hatua hiyo inatokana na changamoto nyingi ambazo amekuwa akikumbana nazo kutoka kwa mashabiki wake ambao wamekuwa wakimsisitiza kufanya hivyo.
Kala ambaye ni zao la Bongo Star Search (BSS) aliiambia Mikito Jumatano kuwa kabla ya mwaka huu kumalizika lazima aikate kiu hiyo kwa kutoa ngoma na kichupa kikali ambacho kitachezwa kwenye runinga za kimataifa.
“Hivi sasa nipo katika harakati za kutoa wimbo mpya utakaoambatana na video kali itakayokuwa na viwango vya kimataifa ili niweze kukata kiu ya mashabiki wangu.
“Kwa sasa siwezi kuweka wazi jina la ngoma hiyo ila nina matumaini kuwa utafanya vizuri, pia video yake nitaifanyia hapa hapa nchini kwa viwango vya kimataifa, namuomba Mungu anijalie uzima ili niweze kutimiza mapema ndoto yangu hiyo,” alisema Jeremiah ambaye alitambulishwa zaidi kupitia Ngoma ya Wimbo wa Taifa aliyofanya na Nakaaya
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE