Rihana yuko kibiashara zaidi, Afungua kampuni ya Urembo na Mitindo


Mrembo mwenye kipaji kikubwa cha kuimba, Rihanna ameanza harakati binafsi za kibiashara baada ya kuanzisha rasmi kampuni binafsi inayojihusisha na Urembo na Mitindo. Kampuni hiyo aliyoipa jina la Fr8me ilizunduliwa rasmi jana. 
Akizungumza na THR Rihanna mwenye umri wa mika 27 alisema "Kutengeneza na kuweka mitindo ya nywele kuna nafasi kubwa katika mitindo.
"Najihusisha kwa karibu sana na hii sehemu ya mikakati yangu, kampuni hii ni kitu cha msingi kwangu kufanya"
Rihanna hajaishia katika hili kwani kwa kushirikiana na Meneja wake anayejulikana kama Benoit Deyoun amefungua kampuni nyingine ya picha inayojulukana kama A Dog Ate My Homework.
Mwimbaji huyo wa Rehab ameshasainisha majina makubwa katika ulimwengu wa mitindo na urembo ambao watakuwa wakifanya kazi chini ya Fr8me wakiwemo Mylah Morales ambaye ndiye msanii wake wa makeup. Wengine ni Taraj P, Jason Bolden, Patricia Morales, Evan Rachel Wood, Fergie na Marcia Hamilton ambaye ni muhudumu wa Jada Pinkett Smith.
"Tumebahatika sana kuwa na watu wenye uwezo mkubwa kwenye masuala ya mitindo na urembo ndani ya Fr8me ingawa nina kamati ndogo ya kusaka vipaji zaidi".
Share on Google Plus

About Mallya Michael

Born in Moshi ,live i Tanga, studied in Arusha, went for military training at Kanembwa in Kigoma & currently pursuing my B.A in Public Relations & Advertising in University of Dar es Salaam