WAJUE MASTAA WANANE WA NIGERIA WENYE MAJUMBA YA KIFAHARI


Genevieve Nnaji
Hili ni jumba la mwigizaji Genevieve Nnaji ambalo alilinunua jijini Accra, Ghana. Jengo hilo lina thamani ya dola milioni nne (Sh. Bilioni 8.6) likiwa eneo la Achimota.
Daniella Okeke
Huu ni mjengo unaotisha wa Daniella Okeke ambao una thamani ya mamilioni.
Ini Edo
Haya ni makazi ya Ini Edo, mmoja wa nyota maarufu wa filamu nchini Nigeria ambako anaishi baada ya kuachana na mfanyabiashara Philip Ehiagwina. Mjengo huo una thamani ya Naira milioni 70 za Nigeria. Mrembo huyo anaishi humo na wadogo zake.
Wasiu Ayinde
Haya ni makazi ya mwigizaji Wasiu Ayinde ambaye anamiliki majumba kadhaa jijini Lagos na mji wa nyumbani kwao huko Ijebu.
Mjengo huu unaoitwa ‘Omoojusagbola House’ ulimalizika kujengwa Machi 2012 wakati akiadhimisha mwaka wa 55 tangu kuzaliwa kwake. Ayinde ambaye anajulikana kama K1 pia ana nyumba jijini Ontario, Canada, ambako mke na watoto wake wanaishi.
Dencia
Haya ni makazi ya kuvutia ya mwigizaji Reprudencia N. Sonkey almaarufu kama Dencia. Mrembo huyo mwenye asili ya Cameroon na Nigeria, ambaye ni mwimbaji, modo, mjasiriamali na mtoa misaada kwa maskini, alilionyesha jengo hilo lililoko Los Angeles, Marekani, ambako anaishi, katika akaunti yake ya Instagram.
Inasemekana utajiri wake unakadiriwa kuwa dola milioni 3.1 au Naira milioni 617 za Nigeria.
Don Jazzy 
Haya ni makazi ya Don Jazzy- Mkurugenzi Mkuu na mmiliki wa Mavin Records ambaye pia ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na prodyuza.
Don ni prodyuza tajiri zaidi wa muziki nchini Nigeria na mwanamuziki anayeshika nafasi ya pili kwa utajiri barani Afrika. Mjengo huu uko eneo linaloitwa Lekki, ukiwa na thamani ya Naira milioni 160 za Nigeria ambapo aliununua mwishoni mwa mwaka 2012.
Chika Ike
Hapa anaishi mwigizaji mrembo Chika Ike eneo la Lekki tangu mwaka 2013 ambapo alinunua jengo hilo kwa mamilioni ya Naira za Nigeria. Katika eneo la jumba hilo kuna bustani, eneo la michezo, ofisi, maegesho ya magari, bwawa la kuogelea na kila aina ya anasa.
Chika Ike ni mmoja wa wanawake matajiri zaidi katika tasnia ya filamu nchini Nigeria. Mbali na mjengo huo pia ana duka linaloitwa Fancy Nancy jijini Abuja.
Timaya
Mwimbaji Timaya ambaye jina lake ni Enetimi Alfred Odom, anaishi hapa katika mjengo huu huko Port Harcout tangu mwaka 2011. Timaya anaishi hapa na binti yake, Emma.
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE