Amarula Kukamua ‘Escape One’ leo Escape one

1Amarula akiwasili Escape One leo kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari.2Amarula akijivinjari maeneo ya  Escape One.
3Meneja Mawasiliano wa Freconic Ideaz, Krantz Mwantepele, akimuongoza Amarula kwenda kuzungumza na wanahabari.
4Amarula akifuatwa nyuma na wanamuziki wake.
5Mkurugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
6Wanahabari wakifanya kazi yao.
7Amarula akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
8Mkutano ukiendelea.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Zambia, Robert Chindaba Banda ‘Amarula’, kesho anatarajiwa kukamua kwenye Ufukwe wa Escape One Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Freconic Ideaz waandaaji wa onesho hilo, Fred Ngimba, amesema baada ya kufanyika Escape One kesho, litafanyika Ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani Dodoma.
Naye msanii huyo aliyeambatana na kundi lake alisema katika maonesho hayo atahakikisha anaonesha makali yake na kuacha gumzo hapa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
Onesho hilo linatarajiwa kusindikizwa na wasanii wa muziki kizazi kipya hapa nchini wakiwemo Benpol, Roma Mkatoliki, Fred Swag, Msouth na wengineo.


PICHA: RICHARD BUKOS / GPL
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE