TDX WANGEX JOINING FLAVOUR ZONE TODAY | 106.5 FM

TDX WANGEX (Wangekewa)

TDX WANGEX maarufu kwa jina hilo ni msanii wa muziki katika miondoko ya HIP HOP kutoka "KASKAZINI" Arusha, ndani ya Tanzania ambaye kwa muda mrefu amekuwa akifanya kazi zake jijini DAR ES SALAAM.

Pia amekuwa akijishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo Kumiliki hisa kadhaa katika maduka ya simu na hatimaye sasa anamiliki Ofisi yake ambaye hujihusisha na uuzaji wa simu, promotion na uuzaji wa copy za mziki na shughuli zinginezo sambamba na hizo inayopatika mtaa wa AGGREY - KARIAKOO.

Katika namna ya utendaji, TDX ni mmoja kati ya wasanii wanaomiliki Copy za ALBUM sokoni pamoja na Singles kwa maana ya wimbo mmojammoja kama ilivyozoeleka hivi sasa kulingana na uwepo wa soko hulia katika mziki ndani ya Tanzania hali iliyotiwa nguvu zaidi na kukua kwa UTANDAWAZI.

TDX WANGEX atakuwa katika studio za MLIMANI RADIO (106.5 FM) kupitia kipindi cha FLAVOUR ZONE kinachoongozwa na KWELI EMCEE kuanzia saa NANE KAMILI (1400) mpaka saaa KUMI KAMILI (1600), akizungumza juu ya kazi yake ya mziki pamoja na changamoto za wazi hususani katika mauzo ya Album katika DIGITAL ERA pamoja na shughuli zinginezo sambamba na mziki wake na maisha kwa ujumla.

Toa mchango wako wa mawazo kupitia:
Facebook : KWELI EMCEE
Twitter : kweliemcee
Google + : +Kweli Emcee 

Share on Google Plus

About KWELI EMCEE

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment