Wateja kutoka mitandao yote kufurahia huduma ya Tigo Pesa ndani ya Tanzania

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha kutoka Tigo, Ruan Swanepoel akiongea kuhusu uzinduzi wa kampeni mpya iitwayo NITIGOPESA, ambayo watumiaji wa huduma za kifedha kutoka mitandao mingine wanaweza kutuma na kupokea pesa kutoka kwa watumiaji wa TigoPesa kwa bei ile ile na wafanyabiashara wanaopokea malipo kwa njia ya Tigopesa sasa wanaweza wakalipwa na wateja wa mitandao mingine bila gharama za ziada, Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga.

Dar es Salaam Juni 28, 2016-Tigo Tanzania  imetangaza kwamba wateja kutoka mitandao yote  hivi sasa wanaweza  kutuma na kupokea  pesa kwa mteja yeyote wa Tigo nchini  kupitia huduma salama na ya uhakika ya Tigo Pesa.
 Hatua hiyo imetangazwa wakati wa  kuzindua kampeni mpya  inayojulikana, ‘NITIGOPESA’ ambayo lengo lake  kuu  ni kuhakikisha wateja kutoka mitandao yote mikubwa ya simu wanaweza kufanya  huduma zao za fedha kwa njia ya simu pamoja na wateja wa Tigo Pesa na wafanya biashara  nchini Tanzania.
 Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Huduma za Fedha, Ruan Swanepoel alisema kuwa Tigo imejikita  kuanzisha  jamii isiyo na tozo  ambapo mteja yeyote  anaweza kufurahia malipo mbadala na kufurahia  huduma  wanazozimudu na za uhakika. Ubunifu huu uliojikita kwa mteja unaangalia ujumuishi wa kifedha kwani unasaidia  kutoa pesa zaidi katika mfumo wa kawaida wa  kifedha na kuchangia katika kuboresha maisha ya wateja kwa kurahisisha shughuli zinazohitaji pesa.
 Alisema kwamba Tigo imewekeza  zaidi ya dola milioni 15 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika kuboresha  jukwaa na huduma zake kufikia ngazi ya kimataifa  ili kuendelea kutoa  huduma zinazofikiwa, za uhakika, salama na sahihi ambapo wateja kutoka mitandao yote  mikubwa ya simu  wataweza kupata muda sahihi na mwitiko usio na kasoro  kutoka huduma ya Tigo Pesa, na hivyo kufanya  shughuli zao za kifedha kufanyika kwa urahisi na kwa kasi.
 “Kuanzia sasa na kuendelea  mitandao mingine ya fedha kwa njia ya simu kama vile M-Pesa, Airtel Money na EasyPesa itaweza kufanya shughuli zake na Tigo Pesa kupitia  ununuzi na ulipaji  kutoka mtandao wetu mpana wa wafanyabiashara wa Tigo Pesa ambao umeenea kote nchini,” alisema Swanepoel.

 Inaweza kurejewa kwamba mwanzoni mwa mwaka huu huduma ya Tigo Pesa ilikamilisha uendeshaji wa pamoja  na waendeshaji wengine wa huduma za kifedha pamoja na mabenki nchini Tanzania katika kuzifanya huduma zake kufikiwa  na watu wengi zaidi.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment