Baada ya Kuandamwa na skendo za Kujiuza, Baby Madaha Abwaga Manyanga Muziki na Filamu.

madaha

IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego  wa kujiuza na makachero wa OFM ya Global Publishers, staa wa Bongo, Baby Madaha ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na  maisha ya presha.

Akistorisha na paparazi wetu juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.

Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa upande wake.

“Nimeamua kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka kutaja), maana naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.
madaha

Hivi karibuni Madaha aliingia kwenye kumi na nane za Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ambapo alipatana bei ya kutoa uroda kwa ‘mfanyabiasha’ wa madini kutoka jijini Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Mike – kumbe ulikuwa mtego.

CREDIT;GPL
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment