MATOKEO SIMBA YA MBEYA CITY 1-1 , LIPULI FC YAICHAPA POLISI MOROGORO 3-1


Mashabiki wa Simba

Matokeo  ya mchezo la  ligi kuu  ya  Voda Com si Simba  wala  Mbeya City  baada ya  timu  hizo  zote  mbili kutoka   uwanjani  hapo kwa kifua mbele  cha goli 1-1.

Mchezo  huo  ambao  kwa Mbeya  City  ni mchezo wa nyumbani  imeweza  kuonyesha umakini mkubwa wa kugomea  kufungwa  katika uwanja  wa Nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya   huku   Simba nayo  ikikwepa " kugagaduliwa " ugenini  kiasi cha kuifanya  Simba  kukomaa na  kusawazisha  goli  la Mbeya  City lililofungwa kipindi cha kwanza huku  Simba ikisawazisha  goli hilo kipindi cha pili .

Timu  ya  Mbeya City ambayo awali  iliweza  kufanya  vema kwa  Yanga  kulazimisha  sare  pia  leo imeweza  kulazimishwa na  Simba  kutoa sare  ya goli 1-1

Wakati   huo  huo timu ya  Lipuli Fc Iringa  imefanikiwa kuichapa timu  ya Polisi  Morogoro  katika mchezo wa  ligi daraja  la kwanza  mzunguko wa  pili kwa jumla ya  goli 3-1

Mchezo huo umechezwa katika uwanja  wa Samora  mjini  Iringa  huku  wadau wa soko  wakiipongeza kwa mchezo  huo.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment