UEFA: Bayern Munich vs Real Madrid,



Gareth Bale tangles with Javi Martinez in first-leg meeting
Bayern Munich watakuwa uwanja wa nyumbani Alianz Arena wakiwakaribisha vijana wa Carlo Ancelot, Real Madrid katika nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Dakika zinahesabika kuelekea katika mchezo huo na homa au presha ya mchezo inazidi kwa makocha, wachezaji na mashabiki wa timu zote mbili.
Katika nusu fainali ya kwanza ambayo ilifanyika nyumbani kwa Real Madrid, pale Santiago Bernabeu, jumatano iliyopita, Real Madrid walifanikiwa kutunza heshima ya uwanja wa nyumbani kwa kuichapa Bayern kwa goli 1-0, goli lililofungwa na Karim Benzema.
Real Madrid wana lengo la kushinda kikombe cha Ulaya kwa mara ya 10 na kucheza fainali yao ya kwanza ya klabu bingwa baada ya kuikosa kwa miaka 12. Misimu mitatu iliyopita Madrid wameshindwa kufuzu kabisa hatua hiyo, wakipoteza dhidi y Dortmund, Barcelona na Bayer Munich ambayo wanakwenda kucheza nayo leo. Timu hizi zilikutana katika hatua hii hii ya nusu fainali miaka miwili iliyopita na Bayern ikafuzu kwa mikwaju ya penalti.
Madrid ina historia mbaya na timu za Ujerumani kwani katika mechi 27 za mashindano ya Ulaya dhidi ya timu za Bundesliga, Madrid imeshinda mechi 2 tu. Faraja waliyonayo Madrid ni kwamba meneja wao Ancelot hajawahi kupoteza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich, hivyo hii inaweza kumpa matumaini ya kutua Lisbon kwa mchezo wa fainali May 24.
Kwa upande wa Bayern wao wanataraji kuwa timu ya kwanza kutetea kombe katika michuano hiyo baada ya kulinyakua mwaka jana. Bayern pia wana rekodi nzuri nyumbani, wakiwa wamepoteza michezo minne peke yake kwa michezo ya msimu mzima na kupata magoli katika michezo 24 dhidi ya michezo 25 ya Ligi ya Mabingwa waliyocheza Alianz Arena.
Timu hizi mbili kihistoria zimeshakutana mara 5 katika hatua ya nusu fainali ya michuano hii na Madrid waliitoa mara 1 Bayern mwaka 2000 na Bayern wameshinda mara 4.
Waswahili wanasema "tusiandikie mate na wino ungalipo" tukatazame mechi. 
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment