Beyonce, Jay Z, Solange "Ndugu wakigombana shikeni jembe mkalime"

Baada ya kuzagaa habari  na video iliyomwonesha Solange Knowles akimshambulia shemeji yake Jay Z katika lifti Jumatatu hii ya May 5 wakitokea Met Gala, wadau wengi wa burudani wamekuwa wakichimbua kupata ukweli wa sababu iliyosababisha sintofahamu hiyo. Wakati watu wakijaribu kuchunguza zaidi, wahusika wakuu wa tukio hilo wamefunguka Alhamisi hii wakiionekana kutuliza soo hilo la kilimwengu. Watatu hao wameripoti kuwa ishu iliyotokea May 5 ni kama ajali tu na wao kama familia wameshaombana msamaha na wamelimaliza suala hilo bila matatizo kama wanafamilia.
Ripoti hiyo imeendelea kutanabaisha kuwa uvumi kuhusiana na ukaidi wa Solange katika jioni ya siku hiyo, hauna ukweli wowote na tatizo hili ni tatizo kama matatizo ya familia zingine, na mwisho wa siku sisi ni familia moja na tunapendana na suala hili lipo katika familia yetu.
Hii inadhihirisha kuwa "ndugu wakigombana wewe shika jembe ukalime"
Share on Google Plus

About Planet Passport

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment