Tasnia ya filamu nchini maarufu kama Bongo Muvi imempoteza mtu muhimu mapema leo alfajiri. Ni aliyekuwa mwongoza filamu na muigizaji Adam Kuambiana.
Ameaga Dunia ghafla akiwa anawahishwa katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuanguka ghafla chooni katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza.
Global Publisher wameripoti kuwa marehemu alilamika sana kuhisi maumivu makali ya tumbo muda mchache kabla ya kukata roho.
Mwanaharakatimzalendo2.blogspot.com inaungana na mamilioni ya Watanzania kuitakia pole familia ya marehemu na Bongo muvi kwa kumpoteza mtu muhimu.
Mwenyezi Mungu ailaze pema roho ya marehemu, Amen!
0 comments:
Post a Comment