AMINI afunguka kilichomfanya afunge Ndoa kimya kimya


Mwanamuziki zao la nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT’, Amini Mwinyimkuu amefunguka kuwa, aliamua kufunga ndoa ya fasta ili kuuwahi mwezi mtukufu wa Ramadhani.
 
Akizungumza na mwanahabari wetu, Amini ambaye amemuoa binti aitwaye  Farida Bashiri alisema ilikuwa vigumu kufanya sherehe kubwa kwani lengo lilikuwa ni kumuingiza ndani haraka mke huyo ili amuandalie futari pia.
amini
“Ni kweli nilioa juzi pale Magomeni Mwembechai, ilikuwa ni ndoa tu na niliamua kufanya hivyo ili kuuwahi mwezi Mtukufu wa Ramadhani,” alisema Amini ambaye ndoa ilimbadili jina kwa kufungishwa kwa jina la Namini kufuata mambo ya kinyota.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment