JOHARI: Baada ya vifo mfululizo wasanii tumenyooka


MKONGWE kwenye sanaa za Kibongo, Blandina Chegula ‘Johari’ amesema kufuatia vifo vya mfululizo vya wasanii, kwa kiasi kikubwa wasanii wamebadilika kitabia.
johari
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, wasanii hao wamejitambua kuwa duniani watu wanapita, jambo ambalo kwa muda mrefu walikuwa wamelisahau na kuponda raha mfululizo.
“Tangu wenzetu wafariki mfululizo, wasanii wengi tumepata mshtuko na kujitambua, naona wengi wamebadilika, wamenyooka na kuanza kumrudia Mungu,” alisema Johari.
Vifo vya wasanii vilivyotokea hivi karibuni ni pamoja na cha Adam Kuambina, Sheila Haule ‘Recho’ na George Tyson.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment