URUGUAY YAANZA VIBAYA, YACHAPWA 3-1 NA COSTA RICA

Costa Rica wakiwashukuru mashabiki baada ya ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Uruguay.
Majonzi: Luis Suarez (wa kwanza kulia) aliyekuwa benchi akiwa haamini kilichotokea.
Edinson Cavani akiifungia Uruguay bao lao pekee.
KIKOSI cha Uruguay kimelala kwa bao 3-1 dhidi ya Costa Rica katika mechi ya kundi D kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2014 zinazoendelea nchini Brazil. Katika mechi hiyo, mshambuliaji mahiri wa Uruguay na Liverpool Luis Suarez alikuwa benchi.
Wafungaji wa Costa Rica waliopeleka maumivu Uruguay ni Joel Campbell, Oscar Duarte na Marcos Urena. Uruguay walipata bao lao kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Edinson Cavani.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment