MANCHESTER United wiki hii wapo tayari kuanza kuifukuzia saini ya kiungo wa Juventus, Arturo Vidal kwa dau la Euro milioni 54.
Klabu hiyo ya Old Trafford
imejiamini kuwa itamnasa nyota huyo wa Chile katika fainali za kombe la
dunia na wanaanza harakati zaidi kumuwinda kiungo huyo mwenye miaka 27.
Louis Van Gaal ambaye
alitambulishwa rasmi kuanza kazi jumatano ya wiki iliyopita, ni shabiki
mkubwa wa Vidal na aliwahi kujaribu kumsajili alipokuwa anafanya kazi
Bayern Munich mwaka 2011 na amethibitisha kumhijtaji tena.
Mholanzi huyo alijaribu
kumshawishi Vidal mapema mwezi Julai, licha ya klabu yake kuambiwa kuwa
itawagharimu Euro milioni 56 jumlisha Luis Nani.
0 comments:
Post a Comment