Diamond uso kwa uso na Davido tena katika tuzo za IRAWMA



Diamond Platnumz na Dabo ni watanzania ambao wamepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika tuzo za kimataifa za muziki wa rege zinazokwenda kwa jina la International Raggae and World Music Awards (IRAWMA). Kwa Diamond hii ni mara ya nne kwa mwaka huu kutajwa kuwania tuzo za kimataifa baada ya zile za MTV MAMA, BET na AFRIMMA na mara hii tena amepangwa kuwania tuzo hiyo na mpinzani wake kutoka Nigeria- Davido. Wimbo mpya wa Diamond "Mdogomdogo" ndio umemwezesha kuingia katika kipengele cha wimbo/mtumbuizaji bora wa Afrika ambapo anachuana na hasimu wake Davido.
Best African Song/Entertainer
 * "Aye" - Davido (Nigeria)
* "Bundeke" - AwiloLongomba (Congo)
* "Tam Tam" - Willy Paul Msafi (Kenya)
* "Sitya Loss" - Eddy Kenzo (Uganda)
* "MdogoMdogo - Diamond" - Platnumz (Tanzania)
* "Mama Africa" - Bracket (Nigeria)
Mtanzania mwingine ni Dabo ambaye ameingia katika kipengele cha chipukizi bora akichuana na wakali wengine kutoka Jamaica na Afrika;
Best New Entertainer:
 * Daniel Bambatta Marley - Jamaica
* MC Norman - Uganda, Africa
* Alkaline - Jamaica
* DABO - Tanzania
* Kranium - Jamaica
* Shatta Wale - Ghana
sherehe za kugawa tuzo hizo ambazo wasanii wengine wakimataifa kama Pharrel Williaams, Chriss brown, Shaggy, Sean Paul na wengine wengi wanawania, zitafanyika huko florida Marekani October 4 mwaka huu.
Upigaji kura umeshaanza na mimi nimeshawapigia Diamond pamoja na Dabo kura, mtanzania ni muda wako wa kudhihirisha uzalendo kupitia www.irawma.com
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment