"HAPPY BIRTHDAY" LOUIS VAN GAAL


Kwa taarifa tu, wakati Tanzania tunasherehekea sikuu ya wakulima maarufu zaidi kama nanenane, Louis Van Gaal ambaye ni kocha wa ManchesterUnited yeye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Mholanzi huyo ambaye amejiunga na mashetani wekundu akitokea kombe la Dunia ambako alikuwa akiinoa timu ya taifa lake, Uholanzi kwa mafanikio, leo anatimiza miaka 63 tangu azaliwe tarehe 8 Agosti, 1951.

Jina kamili la kocha huyo ni Aloysius Paulus Maria van Gaal, ambaye alizaliwa huko Amsterdam, Uholanzi na kuanza kulisakata kabumbu katika nafasi ya kiungo mshambuliaji akivichezea vilabu mbalimbali ikiwemo Royal Antwerp, Telstar, Sparta Rotterdam na AZ . Pia kabla ya kusaini kibarua cha kuinoa Manchester United, Louis Van Gaal amezinoa timu kama  Ajax, Barcelona, AZ, Bayer Munich, na timu ya taifa ya Uholanzi.

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/74396000/jpg/_74396783_vangaalgetty.jpg


Harakati180.blogspot.com inamtakia Van Gaal maisha marefu ,
Share on Google Plus

About Mallya Michael

Born in Moshi ,live i Tanga, studied in Arusha, went for military training at Kanembwa in Kigoma & currently pursuing my B.A in Public Relations & Advertising in University of Dar es Salaam
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment