Diamond Platnamz 'Chibu', baada ya kupata tuzo tatu akiweka heshima ya Bongo Flavour na kuuwakilisha vema mziki huo katika soko la kimataifa akishikilia bendela ya Taifa la Tanzania mgongoni, ametoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu na mashabiki na watanzania kwa ujumla na kusisitiza umoja.
Kupitia ukurasa wake wa facebook Diamond ameandika hivi;
"Kiukweli, haikuwa rahisi kabisa.. lakini kwa uwezo wa
Mwenyez Mungu na support kubwa mliyonipa iliwezesha
Bongo Flavour yetu kuandika Historia mpya kwenye
Ramani ya mziki wa Africa...Hii inaonyesha ni jinsi gani
Umoja ni nguvu na pia jins gani mziki wetu ukisupportiwa
na kupewa kipaumbele unaweza kufika mbali zaidi...
Shukran sana kwa @channeloafrica @channelotv kwa
kuniona na kuthamini kipaji changu, My Family,
Management, Media zote zilizokuwa zikinisupport,
Watangazaji, Wasanii, Wadau na bila kuwasahau wapendwa
wangu #TeamWasafi #TeamChibu #TeamPlatnumz
#TeaMMondi toka instagram, Facebook, Whatsapp, Twitter
na kadharika, wakiongozwa na kamanda langu @kifesi ...
Nawashkuruni sana sana ...najua nikiwatag mimi
wenda nikasahau mmoja, tafadhali naomba nisaidieni
kuwatag hapa waweze kuona shukran zangu kwao...." ameandika Diamond