Mi ni team Kiba lakini napenda mziki wa Diamond – Wema Sepetu

Hivi karibuni Wema alitengeneza vichwa vya habari kwa kuonesha support kubwa kwa Alikiba (hasimu wa Diamond) katika kumuombea kura za KTMA. Kwa wengi hiyo ilitafsiriwa kama kisasi cha Wema kwa ex wake. Na wengine walihisi Kiba na Wema wana lao jambo! Lipi?
wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1
Hata hivyo kupitia kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Jumatatu hii, Wema alisema Kiba ni mtu wake wa karibu tangu siku nyingi na humuita jina la utani ‘bichwa’.
“Ali and I are very good friends,” alisema Wema. “Ali alinitumia meseji kwenye whatsapp akanitumia picha (za KTMA) kama nne, nikamuambia ipi? Akaniambia zote, nikapost zote, akaniambia ntakutumia zingine. Nikamuuliza ‘hivi umetajwa kwenye category ngapi kwenye Kili? Akaniambia saba. Nikamwambia fresh nitumie zote nitakupost. Akaniambia poa na wewe nitumie post zako za Tuzo za watu and I took it as a support, namsupport mshkaji wangu. Mimi ni team Kiba.”
Hata hivyo Wema alisema haoni kama kuna tatizo kama akiwa team Diamond pia.
“I love his [Diamond] music. Mtu akikaa leo akisema kwamba Diamond anaimba vibaya huyo atakuwa ni hater tu, the boy can really sing.”
Source: Bongo5
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE