INI EDO AKOSOLEWA NA MASHABIKI KWA KUJIREMBA ‘VIBAYA’


Staa wa filamu nchini Nigeria, Ini Edo.
Lagos, Nigeria
STAA wa filamu nchini Nigeria, Ini Edo, majuzi alijikuta mashabiki wake wakimtoa makosa kutokana na alivyokuwa amejiremba.
Mashabiki wake hao wanakumbuka pia kwamba mnamo mwaka 2012 wakati wa kuzindua filamu yake na Emem Isong, mwigizaji huyo alionekana kama alikuwa amejiremba harakaharaka.
Jana wakati wa uzinduzi wa filamu za kituo cha televisheni cha MNET jijini Lagos, alionekana katika hali ya “kutisha” kutokana na rangi za macho alizokuwa amezipaka na watu kumshauri atafute mtaalam mwingine wa kumremba.
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE