MUIGIZAJI STAA INI EDO AUCHAPA USINGIZI AKIWA UWANJA WA NDEGE!


MUIGIZAJI STAA INI EDO AUCHAPA USINGIZI AKIWA UWANJA WA NDEGE!

Ini Edo akiwa kauchapa usingizi.
MWIGIZAJI wa Nollywood, Iniobong Edo maarufu kwa jina la Ini Edo ametupia Instagram picha yake akiwa ameuchapa usingizi katika uwanja wa ndege wakati akisubiri kusafiri kwenda mapumzikoni.

Ini akiwa uwanja wa ndege kabla ya kuuchapa usingizi.
Staa huyo wa Nigeria, hakueleza alikuwa anaelekea wapi lakini amesema anakwenda mapumziko na aliwaeleza mashabiki wake kuwa alikuwa na uchovu na usingizi baada ya kusubiri ndege kwa kwa saa 6 na kuwatakia siku njema.

Baada ya kuweka picha yake akiwa amesinzia Ini aliandika na maneno haya.
Katika picha hiyo aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, mashabiki wake walionekana kuvutiwa sana na pete, nywele zake pamoja na saa aliyoivaa mkononi huku wakimsifia mbunifu wake.

Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment