Taylor Swift Amuangukia Nicki Minaj


Mwanamuziki Taylor Swift
Mwanamuziki Taylor Swift
Baada ya kuwepo kwa mvutano mkali kwenye mitandao ya kijamii baina ya Meek Mill dhidi ya Drake pia Nicki Minaj dhidi ya tuzo za MTV VMA’s 2015, Tylor amuangukia mwanadada Minaj na kutaka yaishe.
Hayo yametokea baada ya mitandao mingi kumuunga mkono Nicki Minaj juu ya tuzo za hizo jambo ambalo limepelekea Taylor Swift kumuelewa mwanadada Minaj, kilichomsukuma kukemea ubaguzi kwenye mtandao wa kijamii.
Swift, amenukuliwa kwenye mtandao wa kijamii akiwa ameandika “nilihisi umenishambulia mimi kumbe haiko hivyo, nilikuelewa vibaya..samahani”.
Mwanamuziki Nicki Minaj katika pozi
Mwanamuziki Nicki Minaj katika pozi
Nicki Minaj, alianzisha mjadala kuhusu ubaguzi wa wasanii weusi wa kike kwenye Tuzo za MTV VMA’s huku akidai wasanii wakizungu hupendelewa zaidi, baada ya Taylor kusikia hivyo alimshambulia Nicki na kudai anashangazwa kwa nini yeye yupo mstari mbele kuwachonganisha wanawake kwenye soko hilo.
Baada ya kuelewa nini alichokuwa akijaribu Nicki Minaj, kukipinga Swift, aliamua kuchukua fursa hiyo kumuomba radhi na kuandika “nilihisi nashambuliwa mimi kama mimi, na hasira zilinifanya nisielewe point yako na kunifanya kuongea vile… naomba unisamehe Nicki”.
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE