Zari Ataja Siku Atakayoonesha Sura Ya Mwanae ‘Tiffah’

Mashabiki wa Diamond na Zari wanataka kujua wataona lini sura ya Tiffah mashabiki hao ambao tayari wamekuwa mashabiki wakubwa pia wa mtoto wa mastaa hao, Tiffah Naseeb.
zariii
Zari na Diamond Platinumz wamekuwa wakificha sura ya mtoto wao Tiffah katika mitandao ya kijamii kwa sababu ambazo zinaonekana kufanana na zile walizokuwa nazo mastaa wengine kama Beyonce na Jay Z, Kanye West na Kim Kardashian na kwa Afrika, Tiwa Savage na Tee Billz.
Zarina
Mrembo huyo wa Uganda amejibu swali la mashabiki wao kwa ujumla wakati anajibu swali la shabiki mmoja aliyetaka kufahamu ‘ni lini wataionesha sura ya mtoto wao huyo wa kike’.
“Haudhani kama ni muda sasa wa kuonesha mashabiki wako sura ya mwanao Tiffah?” aliuliza shabiki huy. “Baada ya siku 40,” alijibu Zari.
Zari pia alitumia maneno machache ya Kiganda kujibu tuhuma za King Lawrence aliyetaka wamfanyie Tiffah vipimo vya DNA, “Oyo Mulalu” akimaanisha “huyo niNi Kichaa
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment