MUME AMTETEA JACK WA CHUZI KUKOSA MTOTO
MASKINI! Mume wa mwigizaji wa Bongo Movies, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’, Gadner Dibibi amewataka watu wanaomsema mkewe huyo kuwa hapati mtoto, waache kwani wanajisumbua bure suala hilo ni la Mwenyezi Mungu.
Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’, akiwa na mumewe Gadner Dibibi.
Akizungumza na gazeti hili, Dibibi alisema alipomuoa Jack siyo kwamba alikuwa akifi kiria mtoto ila alijua mtoto analetwa na Mungu hivyo anaamini kuwa watampata tu hivyo amezidisha kumpenda.
“Mtoto ni majaliwa jamani, nilimuoa na nilijua wazi ipo siku Mungu akibariki tutapata mtoto na hata tukikaa miaka kumi bila mtoto siwezi kumuacha mke wangu kwa sababu hiyo, nampenda na nitaendelea kumpenda,” alisema Dibib
Share on Google Plus

About Krantz Mwantepele

#IMAGINE #INSPIRE #INFLUENCE

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment