SAFARI YA CHELSEA KUELEKEA LISBONI, YAISHIA DARAJANI.


Usiku ulioizaa siku ya leo, mashabiki wa soka kote duniani wameshuhudia mchezo mkali dhidi ya vijana wa Mourinho,Chelsea na vijana wa Simeon, Atletico Madrid.Mchuano huo ambao uliziteka hisia za wadau wengi wa soka ulimalizika kwa wageni kuendelea kutamba ugenini katika nusu fainali hizo za ubingwa wa Ulaya.

Baada ya Real Madrid kuilipua Bayern Munich nyumbani Allianz Arena kwa magoli 4-0 usiku wa Jummanne, jana likua ni zamu ya Wahispania tena kutinga fainali baada ya kuisambaratisha ngome ya Jose Mourinho kwa ushindi wa 3-0 pale Stanford Bridge.
Wenyeji The Blues walikuwa wa kwanza kupata goli ambalo lilifungwa na mchezaji wa zamani wa Atletico Madrid, Ferdnando Torres dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza, Torres hakushangilia bao hilo kwa kuonesha heshima ya klabu yake hiyo ya zamani. Bao hilo halikudumu sana kwani dakika 1 kabla ya mapumziko Atletico walipata goli la kusawazisha kupitia kwa Adrian Lopezi.

Dakika ya 54 Mkameruni Samuel Etoo aliingia mchezoni na beki Ashley Cole alikwenda nje,badiliko hili alilifanya Mourinho kwa lengo la kuongeza mashambulizi ili kupata goli la kuongoza, lakini Etoo alioneka kuichimbia kaburi timu yake kwani alisababisha penati dakika 6 baadae kwa kumchezea rafu mshambuliaji wa Atletico, Diego Costa ambaye alikwamisha penati hiyo wavuni kwa ufundi kwa kabisa.

Baada ya Atletico kupata goli la pili walicheza mpira wao wa kiispanyola huku Chelsea wakijaribu kuimarisha mashambulizi kwa kumtoa Torres na kumwingiza Demba Ba. Mabadiliko hayo hayakuifaa kitu Chelsea kwani zikiwa zimesalia dakika 18 ili mchezo uweze kumalizika, Arda Turan aligonga msumari wa mwisho katika jeneza la Chelsea na kuyeyusha malengo ya the Blues kabisa. Na hadi mwamuzi anapuliza filimbi ya mwisho matokeo yalikua ni 1-3. Hivyo fainali itawakutanisha wapinzani kutoka nchi moja na jiji moja la madridi yaani Real Madrid na Atletico Madrid. Mchezo wa fainali utapigwa huko Lisbon, Ureno tarehe 24 May.
Diego Costa katikati akishangilia na wacheaji wenzake baada ya kuifungia timu yake kwa mkwaju wa penati.
Share on Google Plus

About Planet Passport

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment