KELLY ROWLAND AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI
Ni mwezi mmoja tangu mwanadada Kelly Rowland ajifungue mtoto wa kiume, lakini furaha hiyo imeyumba siku ya Jumanne pale mama yake anayefahamika kwa jina la Dorisi alipoaga Dunia.
Mama wa Kelly Rowland amefariki akiwa na miaka 66 huku akiwa amebakisha siku 4 tu kusheherekea miaka 67 ya kuzaliwa yaani Desemba 6.
Mwanamuziki Kelly ameishi zaidi na mama yake baada ya wazazi wake kutalikiana na mama yake kuamua kuwachukua Kelly na kaka yake anayejulikana kama Orlando ambao waliishi Atalanta na baadaye kuhamia Houston ambako ndiko historia ya muziki ya Kelly Rowland ilianzia baada ya kuanza kujihusisha na muziki akiwa na miaka 11 tu.
Akizungumza na vyombo vya habari jana Jumatano mwanamuziki huyo ambaye anaunda kundi la Destiny's Child alisema kwa masikitiko kuwa mama yake alikuwa mtu wa pekee na aliyejitolea mara nyingi kwa ajili ya maisha ya familia yake.
Mungu ailaze roho ya marehemu Doris mahali pema peponi.
0 comments:
Post a Comment