Staa huyo ni Mtunisi ambaye alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo
Manzese Sinza jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, ambapo baada ya
kusomewa shtaka lake la kushambulia mwili, mtuhumiwa alikana na hivyo
hakimu kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena.
Hata hivyo, Mtunisi alishindwa kupewa dhamana baada ya hakimu
kutoridhishwa na afya ya mwanamke huyo, Aziz ambaye anaugulia
nyumbani.Katika hali nyingine, walinzi wa mahakama hiyo walionyesha
mizengwe mikubwa kwa waandishi wa habari hizi, kwa kuwazuia kuingia
ndani ya chumba cha mahakama wala kupiga picha, kwa madai kwamba sheria
zao haziruhusu.
Wakionekana kama waliopewa maelekezo maalum, waliwataka kupeleka
barua kutoka chombo chao cha kazi, kwani hata baada ya kuwakumbusha
kuwa zoezi hilo lilishafanyika siku za nyuma, badala ya kupekua mafaili
yao ili kuiona barua hiyo, waliwataka kwenda kuleta nakala ya barua
iliyoandikwa awali, zoezi ambalo lilikuwa gumu kutokana na muda.
CHANZO
http://www.bongomovies.com
Home / BONGO MOVIES /
FILAMU /
MASTAA /
MTUNISI /
TANZANIA /
VITUKO VYA MASTAA
/ STAA BONGO MOVIE APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUMDUNDA MKEWE
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment