WACHEZAJI CHELSEA WATUA HOSPITALI NA KUTOA ZAWADI ZA KRISMAS


Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Chelsea wamewashitukiza watoto waliolazwa kwenye Hospitali ya Westminster jijini London, England kwa kwenda kuwatembelea pia kuwapa zawadi za sikukuu ya Krismas.



Kundi la wachezaji hao likiongozwa na nahodha John Terry waliibuka hospitalini hapo na kuanza kugawa zawadi kwa watoto waliolazwa.



Hakuna aliyetarajia kuwa Terry pamoja na mshambuliaji Diego Costa, kipa Petr Cech na viungo Ramirez na Fillipe Luis wangeibuka hospitalini hapo kimyakimya.

Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment