Diamond: "nawaheshimu sana wakongwe hawa".



Mafanikio ya mwanamuziki Nasib Abdul maarufu zaidi kama Diamond Platinumz katika muziki wa Bongo Fleva na Afrika kwa ujumla hayafichiki. Mwimbaji huyo wa "Nitampata Wapi" amefanikiwa kupenya katika soko la muziki wa Afrika na kufanikiwa kukomba tuzo kubwa za muziki wa Afrika zikiwemo tuzo tatu za Channel O alizopata mwaka 2014.
 Mbali na mafanikio hayo Diamond sio mnafiki, amekaa chini na kukubali mchango wa wakongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini ambao walimsisimua na kumfanya akaze buti kimuziki. Akiandika katika ukurasa wake wa Facebook amewataja magwiji kama Mr. Nice, T.I.D, Q Chief, Sugu, Dully Sykes, Mr. Blue, Lady Jay Dee, Ray C, Juma Nature na Profesa J. Amemaliza kwa kusema anawaheshimu sana.
Soma hapa post na wasanii aliowataja.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment