Mlinzi wa Liverpool Kolo Toure amethibitisha kustaafu soka la kimataifa na timu ya Ivory Coast, wiki moja baada ya kuisadidia Tembo kushinda Kombe la Mataifa.
Toure ambaye alianza kucheza dhidi ya Rwanda Aprili 2000, alicheza mechi zote sita akihakikisha Ivory Coast ikishinda taji la pili Afrika baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 9-8 dhidi ya Ghana kwenye fainali.
“Naipenda nchi yangu na hasa napenda soka, lakini kwa hatua fulani, kuna muda inabidi uache.”
Akizungumza na vyombo vya habari mjini Abidjan, Toure alisema; “Ni kwa hisia kubwa kwamba nawataarifu kuwa huu ni wakati wa kusema kwaheri.”
“Lengo langu lilikuwa ni kushinda Kombe la Mataifa Afrika na lazima nikubali kwamba ulikuwa uamuzi mgumu kuufanya.”
Toure alikuwa sehemu ya Ivory Coast kwenye Kombe la Dunia mwaka 2006, 2010, na 2014, lakini alicheza mechi moja kwenye fainali za nchini Brazil, kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Ugiriki.
0 comments:
Post a Comment