Msanii Ney wa Mitego amewaambia mashabiki wake juu ya ujio wake mpya wa rekodi yake kali ikiwa ni kolabo na msanii mkubwa kutoka nje ya nchi ambaye amesema kuwa kumtaja sasa si busara mpaka akamilishe baadhi ya mambo.
Ney amesema haya alipo ongea na eatv.tv kuwa anaamini kazi hii itapeleka muziki wa Tanzania mbali.“Mpaka sasa kazi hii imekwishakamilika ikiwa na ladha kutoka Afrika Kusini, Nigeria na hapa Tanzania ambapo imeguswa pia na watayarishaji kutoka ndani na nje ya nchi,” alieleza mkali huyo wa Akadumba.
0 comments:
Post a Comment