Taarifa kwamba muigizaji mrembo wa Ghana Nadia Buari amejifungua watoto mapacha wawili wa kike katika hospitali nje ya nchi zimesambaa Machi 2, 2015.
Taarifa hizo zilithibitishwa na baba yake, Alhaji Sidiku Buari, wengi hawakuamini, huku wengine wakidai ni kama njia ya kutokea na kujitangaza. Hata hivyo, mrembo huyo alithibitisha taarifa hizo siku kadhaa zilizopita, akiwashukuru mashabiki wake kwa upendo wao.
Nadia alijifungua mapacha hao nchini Marekani. Hata hivyo, baba wa watoto hao bado hajajulikana. Tetesi zinazodai anaweza kuwa Jim Iyke zimekataliwa, huku muigizaji akijipanga kumtaja baba wa watoto wake warembo.
Kulikuwa na taarifa hivi karibuni kwamba baba wa mapacha hao ni mtu fulani ambaye alisoma chuo kikuu pamoja naye huku ikidaiwa kuwa mahusiano na Jim Iyke yaliisha baada ya kuchumbiwa mwaka uliopita.
About EDITOR
0 comments:
Post a Comment