Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal mkongwe Thierry Henry amejitetea kupitia kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na uchambuzi wake dhidi ushangiliaji wa mchezaji Javier Hernandez hapo jana usiku.
Thierry katika uchambuzi wake alisikika kwenye kituo cha Super Sport akisema ushangiliaji wa Chicharito ni kama alikuwa ana mshukuru Cristiano Ronaldo.
Nyota huyo wa zamani wa Arsenal inaonekana hakufurahia na ushindi wa klabu ya Real Madrid dhidi ya Atletico kwenye mchezo uliofanyika Santiago Bernabeu.
Hernandez alifunga bao hilo wakati mchezo huo wa ligi ya mabingwa ulaya ukikaribia kumalizika na kuisadia madrid kutinga katika hatua nyingine ya nusu fainali ya mashindano hayo.
About EDITOR
0 comments:
Post a Comment