Mwigizaji Riyama Ally Nae Aonyesha Ujauzito Wake...


Staa wa Bongo Movies, Riyama Ally ambaye ni mama wa mtoto mmoja , hivi juzi kati aliwaacha njia panda mashabiki wake mtandaoni baada ya kuweka picha hiyo akionyesha ujauzito na mpenzi wake akiwa ana ubusu.

Riyama alibandika picha hiyo kuandika “………?” kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kupoteana kabisa, wapo ambao wadai kuwa mwanadada huyo yupo lokesheni anatengeneza muvi na wenngine kudai kuwa hiyo sio muvi bali ni kweli staa huyo kwasasa ni mjamzito.

Kwa siku za hivi karibuni staa huyo amekuwa akitupia picha kadhaakwenye ukurasa wake  akiwa na jamaa huyo (alimuita  Baba Fatma kwenye moja ya posti zake) akimtambulisha kuwa ndio mwandani wake.

BongoMovies.com imejaribu kumtafuta Riyama ili atoboe ukweli juu ya jambo hili bila mafanikio.

Kama ni kweli, tunakupongeza na kukutakia kheri kwani ni jambo jema.

Mzee wa Ubuyu

Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment