WEMA SEPETU " SINA BAHATI NA MARAFIKI KABISA, NAWAPENDA KWA MOYO WOTE ILA WANANIGEUKA..SASA NIMEAMUA KUFUATA USHAURI WA MAMA YANGU"



Na Imelda Mtema
Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu amefunguka kuwa, anajua siku zote yeye hana bahati ya kuwa na marafiki kwa kuwa hata akiwa nao mwishowe kunatokea mgogoro na kuachana huku kila mmoja akimuona mbaya

Akizungumza na gazeti hili juzi, Wema alisema anaumia sana kwa kuwa mara nyingi anawapenda sana rafiki zake kwa moyo mmoja lakini mwisho wa urafiki wao huwa ni mbaya sana tena huvunjika kwa kugombana.

“Mimi nimeshajiona siku nyingi sina bahati kabisa, hata nikiwa na marafiki ambao nawapenda kutoka moyoni, mara nyingi wananigeuka na mama yangu amekuwa akinisihi mara nyingi sana, sasa naona bora nifuate ushauri ambao mama yangu ananishauri wa kuangalia watu wa kuanzisha urafiki nao,” alisema Wema
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment