Ilikuwa wiki iliyopita ambapo mlimbwende na msanii mashuhuri Rihanna alionekana akipata kifungua kinywa na mshambuliaji wa Real Madrid na Ufaransa Karim Benzema baada ya kuhudhuria klabu ya usiki pamoja katika klabu ijulikanayo kama The Griffin Night-Club iliyopo jijini New York. Watu walianza kunong'ona kuwa wawili hawa wanahusiana lakini ikaonekana kuwa ni maneno tuu.Jana wawili hao wameonekana tena huko Hollywood wakiwa pamoja, na vyanzo vingi vya habari vinadai kuwa Rihanna na Benzema walitumia usiku huo wakiwa klabu pamoja ingawa hawakuondoka pamoja.
Tazama video hii kama walivyonaswa na camera za TMZ
0 comments:
Post a Comment