Urafiki wa Wema na Aunt Ezekiel Warejea Kwa Kishindo

Baada ya urafiki wao kuyumba kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili hivi iliyopita, mastaa wa Bongo Movies, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wameonyesha kumaliza tofauti zao na kurudisha urafiki wao kama ilivyo kuwa awali.

Urafiki wa Wema na Aunt ulionekana kuyumba na kufikia hatua ya Wema kutohudhuria baby shower party ya Aunt ambapo Aunt alidai kumualika Wema na hata havi karibuni aunt alipojifungua mtoto Wema hakusema chochote kwenye ukurasa wake mtandaoni ukizingatia kuwa wakati wa ushosti wao alikuwa na kawaidia ya kuweka picha kadhaa za Aunt wakati wa ujauzito na vile vile Wema amakuwa na kawaida ya kuwapongeza mastaa wenzake wakijifungua kupitia ukurasa wake huo.

Kwa kipindi cha miezi hiyo yote, wawili hawa amabo walikua mashosti wa nguvu  hawakuwahi ‘kupostiana’ kwenye kurasa zao kwenye mtandao picha wa Instagram  tofauti na awali. Lakini jana alianza Wema kwa kuweka picha ya Aunt kwenye ukurasa wake na kuandika mistari hii “Ka baby haka....!!!" kisha "Mama Cookie wangu....”

Muda kidogo Aunt naye aliibuka  na kuweka picha ya Wema  na kuandika “Wa kwangu mm Peke yang Mtag bac Mwambie Nampenda mm apa....” Kisha akaweka picha hiyo hapo juu wakiwa wanasukana Aunt aliandika   “My One an Only....Msusi wang mm no saloon “

Kwa mara nyingine wale wapambe nuksi wa Wema na Aunty ambao walikuwa wakisigana kwenye kipindi chote hicho ambacho wawili hao walikuwa hawapo sawa wameumbuka na kuamua kuungana na wadau na mashabiki wengi ambacho wameonyesha kufurahia kitendo cha mashosti hao kuwa karibu kama zamani kwa kumwaga COMMENTS na LIKES za kutosha.

Wapambe ndiyomana mnaitwa NUKSI.
Udaku Special Blog
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment