Pipi aibua mapya adai ‘kushare’ simu na mume wake



Muimbaji wa Bongo Flava, Pipi amedai kuwa yeye na mume wake hutumia simu moja.

Pipi alikuwa akiongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

“Unajua kama mtu sio mwaminifu katika ndoa yako hiyo ndio itakuwa tabu na mtu akiamua kucheat anaweza hata bila simu japo watu wengine wanaona ni wivu lakini hiyo ni misingi ambayo tumejiwekea tokea tulivyoana,” alisema.

“Mimi na mume wangu tuna miaka kumi sasa hivi maana tokea tulivyokuwa hatujafunga ndoa hadi sasa hivi ni miaka kumi inafika. Mimi na mume wangu tuna misingi mizuri ya uaminifu, na wala hatuna mambo mengi kwa hiyo hatuna sababu ya kufichana, kwangu mimi naona ni kawaida tu hata yeye,” aliongeza.
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment