TIGO YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA SHEREHEKEA PESA KWA WIKI YA TISA


Daniel Mruma ni mmoja wa washindi 10 wa wiki ya 9 #SherehekeaPesaNaTigoPesa
Tazama akikabidhiwa na@dogojanjatz na @gnakowarawara zawadi ya hundi ya Mil 1.
Kupitia promosheni hii kila muamala unaofanya unakupa nafasi ya kuwa mmoja wa washindi 10 wa mil 1 kila wiki & mil 10 droo kubwa


Na MWANDISHI WETu

NI wiki ya tisa sasa washindi wa wiki wa Promosheni ya Sherehekea Pesa, inayoendeshwa na Kampuni ya Mawasiliano - Tigo, jana wamejizolea  zawadi zao.

Hadi sasa, Tigo imeshakabidhi, zawadi za jumla ya sh. milioni 90 kwa washindi 90 wa kila  wiki. 

Katika promosheni ya Sherehekea Pesa inayoendelea, washindi 10 hupatikana kila wiki, ambapo kiasi cha zaidi ya sh. milioni 200 zitatolewa kwa washindi wote watakaoibuka kidedea.

Promosheni ya Sherehekea Pesa ni sehemu ya sherehe ya miaka 10 ya kampeni ya Tigo Pesa nchini Tanzania.

Akizungumza jijini Arusha  wakati wa hafla ya kukabidhi fedha, Mkaazi wa Arusha, Daniel Mruma,aliishukuru Tigo,kwa kumkabidhi zawadi hiyo, na kasema ataitumie fedha hiyo kama mtaji wa kuanzia biashara,kwani hajaajiriwa na hana ajira maalum.


"Tunafanya droo hii kila wiki, washindi wanaibuka kidedea kwa kujishindia  fedha taslimu.

“Pamoja na hayo, mteja wa Tigo anavyotumia Tigo Pesa kwa kulipa malipo ya bili, manunuzi ya bidhaa na huduma, kutuma pesa kwa wateja wengine wa Tigo Pesa, kupokea pesa kutoka benki, mitandao mingine na nchi zingine, ndivyo wanavyopata nafasi zaidi kushinda zawadi za pesa. ”  alisema Said Idd, Meneja wa Tigo,Kanda ya Kaskazini

Alisema washindi wa fedha ya kila wiki, wanatoka katika mikoa mbalimbali wanaingia kwenye promosheni hiyo  ya kila wiki ambapo promosheni itaendelea kwa wiki mbili zaidi kutoka sasa na kila wiki washindi 10 watakabidhiwa zawadi zao.

Hadi sasa Tigo imetoa sh. milion 90 na imebakia sh. milion 110 kwaajili ya droo kubwa na washindi wa wiki, itakayofanyika Juni mwaka huu.




Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment