TIGO NA INFINIX WAZINDUA SIMU MPYA MSIMU WA SABASABA


INAKUJA NA OFA: "Simu hii aina ya Infinix Hot 10i inakuja na bei ya Ofa pamoja na GB 78 bureee za kutumia mwaka mzima, ikiwa ni zawadi yetu kwako katika msimu huu wa Sabasaba" Aisha Karupa - Afisa mahusiano Infinix
.

APP YOYOTE! "Infinix Hot 10i imetengenezwa na kupewa uwezo wa kuendesha App yoyote, ikiwemo games za aina mbalimbali" Blass Abdon - Mtaalamu wa bidhaa za Kidigitali, Tigo.
@infinixmobiletz



 Leo tarehe 6 Julai 2021 , Kampuni namba moja ya huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo pamoja na Kampuni ya Simu za mkononi Infinix  wametambulisha simu mpya ya 4G aina ya Infinix HOT 10i. 


Akizungumza wakati wa kutambulisha simu hiyo Mtaalam wa Vifaa vya Mawasiliano kutoka kampuni ya Tigo Bwana Brass Abdon  amesema simu iyo itapatikana kwenye maduka ya Tigo na Infinix Nchi Nzima kwa bei ya Shilingi Laki tatu,  huku ikiwa na Ofa ya Intaneti ya GB 78 kwa mwaka, na kusisitiza juu ya dhamira ya Kampuni ya Tigo kuleta simu hizi nzuri na za kisasa ni kuhakikisha wateja wake wanakwenda kwenye mawasiliano ya Kidigital na kutimiza dhamira ya serikali ya kuhakikisha kwamba kufikia mnamo 2025 asilimia 80 ya vifaa vya mawasiliano vinakidhi TEHAMA kwa mfumo wa Kiserikali. 

Kwa upande mwingine Afisa Mahusiano Infinix Bi. Aisha Karupa amewapongeza Tigo kwa kuendelea kuwa nao bega kwa bega,

"Infinix HOT 10i ni simu ambayo ni rafiki kuanzia bei yake hadi utumiaji , lakini pia simu hii ina kamera mbili (Main Camera ikiwa na Mega Pixels 13 na flash nne,  huku camera ya mbele ikiwa na Mega pixels 8 na flash)  zitakazomfanya mtumiaji kupiga picha nzuri wakati na mahala popote,  lakini pia ina storage kubwa Ya 32 GB na RAM GB 2,  Vile vile inauwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu sana hata kwa zaidi ya siku 2, huku ikiwa na processor bora itayomwezesha mtumiaji kucheza game na kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja maana pia ina kioo kikubwa cha 6.52, nawashauri Watanzania hasa katika msimu huu wa sabasaba watembelee banda la Tigo Infinix tupo hapa kuwahudumia" Alisema Bi Aisha. 

Kufahamu zaidi Tafadhali tembelea kurasa zao za kijamii Tigo na Infinix.

Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment