Kuelekea Brazil: Haya ni matokeo ya mechi za kirafiki za kimataifa

Argentina - Trinidad and Tobago Preview: Albiceleste hope to preserve impeccable home record

Lionel Messi ameingoza Argentina kuiadabisha timu ya taifa ya Trindad & Tobago. Katika mchezo huo uliopigwa  huko Argentina, ulimalizika kwa wenyeji Argentina kupata ushindi wa 3-0.
Argentina wakiwa chini ya kocha mkuu Alejandro Sabella wameweka matumaini ya kufanya vizuri kombe la Dunia ingawa hawajawahi kupita hatua ya robo fainali tangu wapoteze fainali mwaka 1990 kwa kufungwa na Ujerumani 1-0.
Mabao ya Argentina yalifungwa na Palacio dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza, Javier Mascherano dakika ya 51 na Rodriguez akagonga msumari wa mwisho dakika ya 64.

Italy - Luxembourg Preview: Prandelli's men desperate to recover from Ireland upset

Italia kwa mara nyingine tena wamepata sare ya 1-1 wakiwa nyumbani dhidi ya Luxembourg. Vijana wa Prandeli walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 9 kupitia kwa Marcishio kabla ya wageni Luxembourg kusawazisha dakika ya 85 kupitia kwa Chanot.

Ecuador 2-2 England: Rooney & Lambert strike but Three Lions falter in Miami

Waingereza walipata droo pia lakini wao wakiwa wamesafiri hadi Ecuador ambako walicheza na timu ya taifa hilo.Wenyeji Ecuador walikuwa wa kwanza kuliona lango la Uingereza kupitia mshambuliaji wao Enner Valencia.
Uingereza walipumua kupitia kwa Wayne Rooney dakika ya 29 baada ya kufunga goli la kusawazisha. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa matokeo ya 1-1, kipindi cha pili Uingereza walipata goli la kuongoza dakika ya 51 kupitia kwa Rickie Lambart kabla ya wenyeji kusawazisha dakika ya 70 kupitia kwa Michael Arroyo na matokeo kuwa 2-2.
Decisive: Arjen Robben scored one and made one for Holland in their win against Wales

Uholanzi wameshinda mechi yao ya kirafiki dhidi ya Wales kwa magoli mawili ya Arjen Robben na Jeremain Lens.
Share on Google Plus

About Planet Passport

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment