MTV MAMA Awards 2014, ni kesho ndani ya Durban, Diamond Platnumz ni mmoja ya watumbuizaji.

Baada ya kupiga kura kwa wanamuziki mbalimbali wanaowania tunzo hizo, umewadia wakati wa kushuhudia sherehe za ugawaji tunzo hizo za MTV MAMA kwa mwaka huu wa 2014.
Sherehe hizo zitafanyika kesho tarehe 7 katika jiji la Durban nchini Afrika Kusini.
Watumbuizaji kutoka Bara la Afrika wametajwa na Diamond kutoka Tanzania akiwemo, wengine ni Wizkid kutoka Nigeria, Phyno wa Nigeria, na Yuri Da Cunha kutoka Angola.
Wasanii ambao walitangulia kutajwa kama watumbuizaji katiaka sherehe hizo kutoka Afrika na Davido wa Nigeria na Mafikizolo wa Afrika Kusini.
post title

Wanamuziki wa kimataifa kutoka nje ya Afrika ambao wametajwa na MTV kupagawisha katika sherehe hizo siku ya kesho ni pamoja na mkali Trey Songz kutoka Marekani, 2014 MAMA Performers

French Montana naye kutoka maandishi matatu atatumbuiza:
2014 MAMA Performers

Miguel,mkali mingine wa R&B kutoka Marekani atakuwepo kusherehesha katika sherehe za tunzo hizo;
2014 MAMA Performers

MC katika sherehe hizo ni muigizaji na mchekeshaji nguli kutoka nchini Marekani ajulikanaye kwa jina la Marlon Wayans.

post title

Mtanzania Diamond Platnumz ana rekodi katika tunzo hizo akiwa manamuziki wa kwanza kutoka Tanzania kushiriki katika tunzo hizo za MTV MAMA. Kila Mtanzania anamwombea Diamond Platnumz dua njema, baada ya kumpigia kura aweze kuibuka na tunzo zote mbili katika vinyang'anyiro vyote viwili anavyowania. Vinyang'anyiro hivyo ni vya Best Male na Best Collaboration.




Share on Google Plus

About Planet Passport

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment