Nooij amtema Ngassa Taifa Stars


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij.
Na Khadija Mngwai
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij, amemuondoa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa katika kikosi chake kitakachoivaa Msumbiji.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga na timu ya Taifa Stars, Mrisho ngassa.
Sababu kubwa iliyotajwa ni Ngassa kushindwa kuripoti katika kikosi hicho wakati alipoitwa kucheza dhidi ya Botswana kabla ya kuivaa Msumbiji katika kuwania kushiriki Kombe la Mataifa Afrika (AFCON).
Chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la Stars, kimesema kuwa Ngassa alikaidi wito wa kocha huyo, ndiyo maana akamkasirisha.
“Kocha hatamtumia Ngassa katika mechi ijayo dhidi ya Msumbiji,” kilisema chanzo hicho. Alipoulizwa Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa alisema hawana taarifa yoyote juu ya kutokuwepo kambini kwa mchezaji huyo.

“TFF haihusiki kwa namna yoyote juu ya kuondoka kwa Ngassa, kwani mamlaka yote yapo kwa klabu yake ambayo ndiyo inammiliki,” alisema Mwesigwa.
Maximo kuwaongoza mashabiki Yanga kuishangilia
Share on Google Plus

About EDITOR

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment