HABARI YA KUSIKITISHA: MSHIRIKI WA AMERICAN IDOL "MICHAEL JOHNS" AFARIKI


michael johns

Kwa wafuatiliaji wa mashindano ya kuimba ya American Idol ya huko nchini Marekani, Michael Johns siyo jina jipya masikioni mwao. Michael Johns aliwahi kushiriki mashindano hayo ya kuibua vipaji na kufanikiwa kufika season ya 7 mwaka 2007 akimaliza katika nafasi ya 8. Baada ya kutoka katika mashindano hayo Michael Johns aliamua kurekodi album yake mwenyewe inayoitwa "Hold Back My Heart" mwaka 2009.
Kwa mujibu wa TMZ inasadikika kuwa mwanamuziki huyo alifariki jana Ijumaa akiwa anasumbuliwa na maumivu ya kisigino.
Johns amefariki akiwa na umri wa miaka 35. Tazama moja ya vipande wakati akiimba katika mashindano ya American Idol:

Roho ya marehemu ilazwe mahali pema.

Share on Google Plus

About Mallya Michael

Born in Moshi ,live i Tanga, studied in Arusha, went for military training at Kanembwa in Kigoma & currently pursuing my B.A in Public Relations & Advertising in University of Dar es Salaam
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment