Man U yamtangaza rasmi Marcos Rojo




Luis Van Gaal ameongeza nguvu katika kikosi chake cha Manchester United baada ya kumsajili beki aliyefanya vizuri katika kombe la Dunia la Brazil akiichezea Argentina, Marcos Rojo. Rojo amejiunga na klabu hiyo ambayo imeanza msimu kwa kupoteza dhidi ya Swansea kwa kitita cha Euro milioni 20 akitokea klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno na kusaini mkataba wa miaka mitano.
Wakati Muargentina huyo akijikita katika kikosi cha mashetani wekundu, winga Luis Nani atajiunga na Sporting Lisbon kwa mkopo.
Rojo ambaye ni mchezaji wa tatu kusajiliwa na mdachi Van Gaal ameichezea timu yake ya taifa ya Argentina michezo 28 ikiwemo sita ya kombe la Dunia la mwaka 2014. Baada ya kukamilisha vipimo  mapema leo na kutangazwa jioni hii Rojo alisema "Ni heshima kubwa kusema naichezea Manchester United. Ligi kuu ya Uingereza ndio ligi inayovutia zaidi, na kuichezea klabu kubwa Duniani kama United ni ndoto kwangu. Mimi ni kijana na bado nina morali ya kuendelea kujifunza soka, kuwa chini ya kocha mzoefu na mwenye ufundi kama Van Gaal ni ngekewa kwangu. Nimejiunga na United ili kushirikiana na wachezaji wenzangu tuweze kutwaa vikombe, na nadhani hata kocha ana lengo kama langu".
Kwa upande wa kocha Van Gaal alisema "Rojo ni beki aliyebarikiwa. Ameshafika mbali kisoka na anaweza kucheza kama mlinzi wa kati au wa kushoto. Ana uwezo, nguvu na nia ya kujifunza, hii inamaanisha kuwa ana malengo mazuri. Alicheza kwa kiwango kizuri kombe la Dunia na pia amecheza Ulaya miaka kadhaa. Ni nyongeza nzuri katika kikosi".
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment